NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 17

Somo la 17

Pendekezo lako ni lipi?

Kwenye duka la vitabu, Anna ameona vitabu vingi vya manga ambavyo vinaonekana kumvutia. Hawezi kuamua ni kipi atakachokinunua.

Somo la 17 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

OSUSUME WA NAN DESU KA

Mazungumzo

アンナ あ、この本いいなあ。あれも面白そう。 Ah! Kitabu hiki ni kizuri. Kile pia kinaonekana kuvutia.
Anna A, KONO HON II NÂ. ARE MO OMOSHIROSÔ.
Ah! Kitabu hiki ni kizuri. Kile pia kinaonekana kuvutia.
アンナ さくらさんのおすすめは何ですか。 Sakura, pendekezo lako ni lipi?
Anna SAKURA-SAN NO OSUSUME WA NAN DESU KA.
Sakura, pendekezo lako ni lipi?
さくら これはどう? Unaonaje kuhusu hiki?
Sakura KORE WA DÔ?
Unaonaje kuhusu hiki?
アンナ ホラーはちょっと…。 Simulizi za kutisha kidogo mimi aah....
Anna HORÂ WA CHOTTO....
Simulizi za kutisha kidogo mimi aah....

Vidokezo vya sarufi

  WA CHOTTO

Unaweza kusema hivi kukataa pendekezo kwa namna ya kiungwana, ama isiyo ya moja kwa moja.
k.m.) HORÂ WA CHOTTO.... (Simulizi za kutisha mimi kidogo aah....)

Mwalimu Tufundishe

Kivumishi + SÔ
OMOSHIROSÔ, ni "Inaonekana kuvutia."

Tanakali Sauti

Ukimya / Kujipanga kwenye mstari
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Duka kubwa la vitabu lina tarakilishi za kutafutia vitabu kwa ajili ya wateja. Tunaweza kuzitumia kutafuta ikiwa duka husika lina kitabu fulani unachotafuta na wapi kilipo.
Ni jambo linalorahisisha mchakato wa utafutaji vitabu.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.