NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 14

Somo la 14

Naweza kutupa taka hapa?

Anna anafanya usafi baada ya karamu iliyofanyika katika bweni lao.

Somo la 14 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

KOKO NI GOMI O SUTETE MO IIDESU KA

Mazungumzo

アンナ お母さん、ここにゴミを捨ててもいいですか。 Mama, naweza kutupa takataka hapa?
Anna OKÂSAN, KOKO NI GOMI O SUTETE MO II DESU KA.
Mama, naweza kutupa takataka hapa?
寮母 そうねえ。缶は別の袋に入れてください。資源ですから。 Aha. Tafadhali weka makopo kwenye mfuko mwingine. Kwa sababu ni rasilimali.
Msimamizi wa bweni SÔNÊ. KAN WA BETSU NO FUKURO NI IRETE KUDASAI. SHIGEN DESU KARA.
Aha. Tafadhali weka makopo kwenye mfuko mwingine. Kwa sababu ni rasilimali.
アンナ はい、分かりました。 Naam, nimeelewa.
Anna HAI, WAKARIMASHITA.
Naam, nimeelewa.

Vidokezo vya sarufi

KARA

Katika muktadha huu, KARA inaonyesha sababu.
k.m.)  SHIGEN DESU KARA, BETSU NO FUKURO NI IRETE KUDASAI. (Kwa sababu hizo ni rasilimali, tafadhali uziweke kwenye mfuko mwingine.)

Mwalimu Tufundishe

Kitenzi cha umbo la TE + MO II DESU KA
Ikiwa kitenzi cha umbo la TE na MO II DESU zinatamkwa kwa pamoja, inamaanisha ya kwamba ombi la ruhusa limekubaliwa.

Tanakali Sauti

Kuchoma
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kuna masharti ya kina kuhusiana na suala la kutenganisha takataka. Ni lazima tuoshe makopo na chupa za plastiki kabla ya kuzitupa. Nitajitahidi, kadiri ya uwezo wangu.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.