NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 13

Somo la 13

Ninapenda riwaya.

Anna, Sakura na Rodrigo wanaendelea na mazungumzo kwenye karamu, inayofanyika kwenye bweni la wanafunzi wa kigeni.

Somo la 13 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

SHÔSETSU GA SUKI DESU

Mazungumzo

さくら ロドリゴさんの趣味は何ですか。 Rodrigo, unapenda nini?
Sakura RODORIGO-SAN NO SHUMI WA NAN DESU KA.
Rodrigo, unapenda nini?
ロドリゴ 読書です。特に歴史小説が好きです。 Kusoma vitabu. Ninachopenda hasa ni riwaya za historia.
Rodrigo DOKUSHO DESU. TOKUNI REKISHI SHÔSETSU GA SUKI DESU.
Kusoma vitabu. Ninachopenda hasa ni riwaya za historia.
さくら へえ。新宿に新しい本屋が出来ましたよ。
みんなで行きませんか。
Aha! Kuna duka jipya la vitabu limefunguliwa Shinjuku.
Kwa nini tusiende pamoja?
Sakura HÊ. SHINJUKU NI ATARASHII HON-YA GA DEKIMASHITA YO.
MINNA DE IKIMASEN KA.
Aha! Kuna duka jipya la vitabu limefunguliwa Shinjuku.
Kwa nini tusiende pamoja?

Vidokezo vya sarufi

A WA B GA SUKI DESU

(A anapenda B.)
SUKI ni kivumishi kinachomaanisha "kupenda." GA inaonyesha mtendwa.
k.m.) ANNA WA MANGA GA SUKI DESU. (Anna anapenda katuni za manga.)

  MASEN KA

Ikiwa utabadilisha MASU iwe MASEN KA, unawataka watu wafanye jambo fulani pamoja.
k.m.)  MINNA DE HON-YA NI IKIMASU. (Tutaenda kwenye duka la vitabu pamoja.)
>>MINNA DE HON-YA NI IKIMASEN KA. (Unaonaje tukienda kwenye duka la vitabu?)

Mwalimu Tufundishe

Aina mbili za vivumishi
Kuna vivumishi vya aina mbili. Vile vinavyomalizikia na silabi I, na vile ambavyo havimalizikii na silabi hiyo. Vile vinavyomalizikia na silabi I vinaitwa vivumishi vya I. Vinajumuisha HIROI (pana), na ATARASHII (mpya).

Tanakali Sauti

Kung'aa
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Rodrigo ni mtu wa kupigiwa mfano. Anaonekana kana kwamba anasoma riwaya za Kijapani. Nitajitahidi ili na mimi niweze kusoma katuni za manga za Kijapani!

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.