Herufi za Kijapani

Lugha ya Kijapani ina aina tatu za herufi: Hiragana, Katakana na Kanji.
Herufi za Hiragana na Katakana ni alama za kifonetiki, kila moja inawakilisha silabi moja wakati herufi za Kanji ni idiogramu, kila herufi moja ya Kanji inakuwa na maana fulani.