NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Tunajifunza na Anna!

Tafadhali piga picha inayoonyesha jinsi unavyojifunza Kijapani, ututumie!

[Vigezo na masharti ya kutuma]

  • Hatuwezi kukuhakikishia kwamba picha na maoni yote utakayotutumia vitatangazwa ama kuwekwa kwenye tovuti.
  • Tafadhali hakikisha kuwa ukubwa wa taarifa kwenye faili utakalotutumia hautazidi 200MB.
  • Bila kujumuisha anuani za barua pepe, maudhui ya taarifa zitakazokusanywa kupitia tovuti hii, ikiwemo matokeo ya ukusanyaji taarifa, vinaweza kutangazwa kwenye matangazo ya ndani ya Japani ya NHK, pamoja na marudio yake, ambayo yanajumuisha utumiaji wa taarifa hizo kwa namna nyingine. Pia vinaweza kutumika kwenye matangazo ya NHK ya kimataifa, kutumika nje ya nchi na shughuli kama za uhusiano kwa umma, kutumika katika mashindano ya vipindi, matukio, maktaba za wazi na tovuti, bila kujali ikiwa fidia italipwa au la. Vinaweza pia kutolewa kwa vituo vingine vya matangazo ya ndani ya Japani na ya kimataifa mbali na NHK, runinga za ndani ya Japani pamoja na warushaji wa matangazo nje ya Japani, na vinaweza kutumika kwa ajili ya video za biashara ama bidhaa za sauti, na kutolewa kama nyenzo za uaandaaji wa video na sauti, machapisho na tovuti. Pia fahamu kwamba taarifa hizo zinaweza kutumiwa bila mtumaji kupewa taarifa ya awali.
  • Jina lililotumiwa wakati wa kutuma linaweza kuondolewa kwa malengo yaliyotajwa hapo juu.
  • Picha na maoni uliyotutumia vinaweza kubadilishwa na kufupishwa na wahariri bila kuathiri makusudio ya mtumaji na maudhui ya maoni yake.
  • Tafadhali usitumie kazi ya mtu mwingine mbali na wanaoonekana kwenye picha na kutajwa kwenye maoni. Hii inajumuisha michoro, picha, nukuu za sentensi kwenye kazi nyingine na mashairi.
  • Ikiwa mtu mwingine atalalamika kuhusu uwezekano wa ukiukwaji wa haki kuhusiana na picha au maoni yaliyotumwa, mtumaji atawajibika kikamilifu.
  • Ikiwa mtumaji ni mtoto kwa mujibu wa sheria za nchi yake, mtumaji atapaswa kupata idhini kutoka kwa mlezi wake.
  • Tafadhali kumbuka kuwa, taarifa zilizotumwa haziwezi kurejeshwa.
  • Anuani za barua pepe zilizotumwa zitatumika kwa minajili ifuatayo pekee.
    1. (1) Kuwasiliana kwa ajili ya kuuliza maswali kuhusu picha au maoni yako
    2. (2) Kuwasiliana kuhusu maandalizi ya kipindi
    3. (3) Kukutaarifu kuhusu kutolewa kwa kipindi, picha au maoni yako kutumika kwenye shughuli nje ya zile za NHK
    4. Hazitatumiwa kwa malengo mengine
  • Kuhusu jinsi NHK inavyoshughulikia taarifa binafsi, tafadhali soma "Kuhusu sera ya NHK juu ya Ulinzi wa taarifa binafsi."

Tafadhali tuma picha yako na maoni ikiwa unakubaliana na masharti yaliyoorodheshwa hapo juu.