NHK WORLD

Alhamisi, Machi 26, 2020

Tebako (kasha la vipodozi) Mapambo ya magurudumu kwenye mto katika mbinu ya Maki-e na vipande vya makombe
(Katawaguruma Maki-e Raden Tebako)

Vipindi vilivyotangulia

Utangulizi

Kila kazi bora ya sanaa, iwe mchoro au uchongaji, ina simulizi inayovutia watu. Kufahamu simulizi hizo ni hatua ya kwanza ya kuelewa kile kinachowavutia watu. Katika kipindi hiki, tutatambulisha baadhi ya kazi za sanaa zilizopo kwenye Makumbusho ya Taifa ya Tokyo, ili kufahamu siri ya kazi hizo.

Makumbusho ya Taifa ya Tokyo

Makumbusho ya Taifa ya Tokyo

Ikiwa imejengwa mwaka 1872, makumbusho ya Taifa ya jijini Tokyo ni ya zamani zaidi nchini Japani. Kwa wakati huo Japani ikiwa ni nchi masikini, ilizatiti nguvu zake zaidi kujenga makumbusho, kama sehemu muhimu ya juhudi za kubadilika kwenda kwenye usasa. Tangu wakati huo kwa zaidi ya miaka 140, makumbusho hiyo imekusanya kazi za sanaa na nyaraka za kihistoria na kazi za zamani za mataifa ya Asia hususani Japani. Makumbusho hiyo pia hufanya tafiti kuhusu kazi ilizokusanya. Hutunza na kukarabati kazi za sanaa na kuzionesha. Pia makumbusho hiyo hufanya shughulimbalimbali za kielimu, na hivi sasa ina zaidi ya kazi za sanaa 110,000.